Thursday, 18 December 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO DESEMBA 18,2025

 Magazeti







Share:

Wednesday, 17 December 2025

WAZIRI MCHENGERWA KUSHIRIKI MKUTANO WA DUNIA KUHUSU TIBA ASILI, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAWAZIRI WA AFYA


Na John Mapepele, New Delhi

Waziri wa Afya wa Tanzania, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa amewasili New Delhi, nchini India, tayari leo kushiriki Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu tiba asili ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Tanzania katika kushirikiana na mataifa mbalimbali kwenye kuboresha huduma ya afya kwa wananchi ambapo amepokelewa na ujumbe wa ubalozi wa Tanzania India ukiongozwa na Mhe. Balozi, Anisa Mbega.

Mkutano huu wa kimataifa unaoratibiwa moja kwa moja WHO kwa kushirikiana na Serikali ya India unajumuisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wasimamizi wakuu wa sekta ya afya katika nchi mbalimbali hususan mawaziri watunga sera wakuu, na wataalam wa fani tofauti lengo likiwa ni kujadili nafasi ya tiba asili katika kuimarisha mifumo ya huduma za afya.
Akiongea mara baada ya kuwasili jijini New Delhi, Mhe. Mchengerwa amesema miongoni mwa mambo makubwa yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na utawala na udhibiti wa tiba asili, utafiti na Ushahidi wa kisayansi, ujumuishaji wa tiba asili katika mifumo ya afya, matumizi endelevu ya raslimali za kiasili, uendelezaji wa raslimali watu, pamoja na ushirikiano wa kimataifa sambamba na mkakati wa WHO wa Tiba qhTanzania katika mkutano huo katika kipindi hiki unaonesha dhamira ya Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tiba asili inaendeshwa kwa kuzinngatia, Ushahidi wa kisayansi, usalama na mifumo madhubuti ya udhibiti kama sehemu za kuimarisha huduma za afya, na kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma ya afya kwa wote nchini.

Pia hivi karibuni wakati wa kikao kazi na wafanyakazi wa Taifa ya Muhimbili Mhe Mchengerwa alitoa dira ya Wizara yake huku akiainisha maeneo sita ya mageuzi yanayolenga kuipeleka Sekta ya Afya katika viwango vya juu ili kuwakomboa wananchi kwenye eneo la afya huku akipigia msumari wa moto maelekezo mahususi ya Mhe. Rais Samia ya kuanzisha Bima ya Afya kwa wote, kuhakikisha wagonjwa wasio na uwezo wanaendelea kupatiwa huduma zote za afya bila kikwazo cha fedha, pia hospitali zote nchini zinaacha mara moja kuzuia maiti kwa sababu za kudaiwa gharama za matibabu.
Kando ya mkutano huo, ubalozi wa Tanzania nchini India umeandaa mikutano na vikao vya mazungumzo vinavyolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kati ya Tanzania na India, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa usainiwaji wa hati ya makubaliano (MoU) kuhusu ushirikiano katika mfumo wa tiba asili ya Ayurveda ya India kati ya Wizara ya AYUSH ya Serikali ya India na Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Share:

DKT. MWIGULU ASHIRIKI MAZISHI YA MHE. JENISTA MHAGAMA


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, aliposhiriki Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Desemba 16, 2025. Mazishi yaliongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi. (Picha na Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, aliposhiriki Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Desemba 16, 2025. Mazishi yaliongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (Picha na Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi aliposhiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Desemba 16, 2025. (Picha na Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na waombolezaji aliposhiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Desemba 16, 2025. Mazishi yaliongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (Picha na Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu)
Share:

MAJIBU YA UPOTOSHAJI KUHUSU MAENDELEO YA TANZANIA


 Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uswidi, Benjamin Dousa, tarehe 5 Desemba, alitangaza uamuzi wa Serikali ya Uswidi kufuta misaada kwa nchi tano za Tanzania, Msumbiji, Zimbabwe, Liberia na Bolivia baada ya kupitia vipaumbele vya kisera na changamoto za kiusalama. 

Hata hivyo, wakati akitoa tangazo hilo, alizisakama nchi hizo kwamba zimekwama katika ujamaa na kushindwa kuendelea. 

Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, anajibu kwa kuelezea mafanikio ambayo Tanzania imefikia katika maendeleo ya uchumi kwa miaka 60 iliyopita. 

Hii ni tafsiri ya makala hii iliyochapishwa tarehe 16 Desemba, 2025, kwenye gazeti la Aftonbladet kwa lugha ya Kiswidi.

Na: Balozi Mobhare Matinyi

Serikali ya Uswidi tarehe 5 Desemba, baada ya kupitia vipaumbele vyake vya sera za mambo ya nje na changamoto za kiusalama, ilitangaza uamuzi wa kufuta misaada yake ya ushirikiano wa maendeleo na nchi tano kabla ya mwisho wa mwaka 2026, na hivyo kuhitimisha misaada iliyodumu kwa miongo kadhaa.

Moja ya nchi zilizoathiriwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nchi ambayo imedumisha uhusiano mzuri na Uswidi tangia miaka 62 iliyopita. Kufanana katika itikadi ya demokrasia ya  kijamii kati ya nchi hizi mbili ndiko kulikozaa uhusiano huu wa kipekee. 

Waumini wa demokrasia ya kijamii huamini katika haki ya kijamii, uhuru, usawa, utu wa binadamu na mshikamano ndani ya mfumo wa demokrasia unaoruhusu serikali kuingilia ubepari ili kuwezesha ustawi wa jamii.

Hata hivyo, wakati Uswidi ikiwa na demokrasia ya vyama vingi na kujali ustawi katikati ya ubepari, Tanzania ilichagua kufuata mfumo wa demokrasia ya chama kimoja kinachofuata Ujamaa wa Kiafrika ambayo ilisisitiza kujitegemea. Uswidi hivyo basi, ikachukua jukumu la kuwa mkufunzi wa harakati za vyama vya ushirika kwa Tanzania wakati huo.

Nchi hizo mbili zilikuwa zikitofautiana katika maendeleo ya kiuchumi kwa kiasi kikubwa kwani Uswidi iliyokuwa na watu milioni 7.5, ilikuwa na Pato la Taifa la dola za Marekani bilioni 17.33 mwaka 1961, huku ikiendesha uchumi imara wa viwanda wakati Tanzania iliyokuwa na watu milioni 10.3 ilikuwa na Pato la Taifa la dola za Marekani bilioni 2.83 huku ikitegemea zaidi uchumi wa kilimo. 

Kwa hiyo Uswidi, mwaka 1963, iliona umuhimu wa kuiunga mkono Tanzania, wakati huo Tanganyika kabla ya kuungana na Zanzibar mwaka 1964 na kuunda Tanzania, kwa sababu nchi hiyo mpya ilikuwa imeonyesha dira makini ya maendeleo chini ya Rais Julius Nyerere.

Tangazo la hivi majuzi la Serikali ya Uswidi, bila kukusudia, liliibua simulizi iliyoipotosha taswira ya Tanzania na mafanikio yote ya ushirikiano huu wa fahari. Ilidaiwa kuwa nchi zilizotajwa "zimekuwa zikifuata Ujamaa mno" kwa miongo mingi na matokeo yake "hazijaendelea". 

Niseme wazi vizuri kabisa: Kauli hiyo haiendani na Tanzania kwa namna yoyote ile, hata kwa fikra tu.

Hebu tuangalie ukweli: Mwanzoni mwa miaka ya 1960 Tanzania ilikuwa na chuo kikuu kishiriki kimoja tu, lakini leo ina vyuo vikuu 36 vilivyosajiliwa na vyuo vikuu vishiriki 16. Uswidi, kwa upande wake, leo ina vyuo vikuu 18 vilivyosajiliwa na vyuo vikuu vishiriki 12. Kwa hakika, ikiwa na takribani watu milioni 70, Tanzania bado inahitaji vyuo vikuu zaidi ikilinganishwa na Uswidi yenye milioni 10.7.

Wakati huo Tanzania ilikuwa na vituo kutolea huduma za afya 1,343 zikiwemo hospitali 96 na vituo vya afya 22. Leo Tanzania ina vituo vya aina zote vya kutolea huduma za afya 13,606 zikiwemo hospitali 473 na vituo vya afya 1,348. 

Tunashukuru kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Chuo Kikuu cha Karolinska ya jijini Stockholm na Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyo pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Tanzania ilianza na uwanja wa ndege wa kimataifa mmoja jijini Dar es Salaam lakini imeongeza viwanja viwili Kilimanjaro na Zanzibar na vingine viwili Dodoma na Mwanza vikiendelea 

kujengwa. Nayo Uswidi ina viwanja vya ndege vya kimataifa vikubwa zaidi huko Stockholm, Gothenburg na kidogo cha Malmo.

Ikiwa katika ukanda wa kimkakati wa mwambao wa Afrika Mashariki, Tanzania inahudumia nchi kadhaa zisizo na bandari kupitia bandari zake kuu nne za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga na Zanzibar, na hivi karibuni itaanza ujenzi wa bandari kubwa ya Bagamoyo. Pia kuna bandari kadhaa kwenye maziwa makuu matatu ya Afrika, Victoria, Tanganyika na Nyasa. 

Mtandao mkubwa wa barabara na reli wa Tanzania ni miongoni mwa mitandao yenye ufanisi mkubwa barani Afrika na unaendelea kukua. Tunaipongeza Serikali ya Uswidi kwa kuunga mkono kwa njia mbalimbali mradi wetu wa reli ya kisasa (SGR), reli ya kwanza inayotumia umeme Afrika Mashariki na Kati. 

Kwa sasa reli hiyo inafanya kazi kati ya Dar es Salaam na mji mkuu Dodoma. Miradi zaidi ya reli katika maeneo ya kaskazini na kusini mwa nchi, ambayo kimsingi itaunganisha nchi zaidi na bahari ya Hindi, iko mbioni.

Baada ya miaka michache, Tanzania itakuwa kitovu kikubwa cha nishati baada ya kukamilisha mradi wa gesi asilia na kampuni ya Norway, Equinor, wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 42.

Aidha, mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki linaloanzia Uganda hadi bandari ya Tanga unakaribia kukamilika.

Vilevile, Tanzania, ambayo inazalisha maelfu ya megawati za umeme kwa kutumia mitambo ya nguvu za maji, imejiandaa vizuri kutumia vyanzo vingine vya nishati mbadala kama jotoardhi, upepo na jua. 

Kadhalika, Tanzania ina akiba kubwa ya makaa ya mawe inayokadiriwa kufikia tani bilioni 1.9.

Mtazamo wa uchumi wa Tanzania pia ni wa kuvutia. Ingawa Pato lake la Taifa linakaribia dola bilioni 90, ukuaji wa uchumi kama inavyoshuhudiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Mikopo ya Mauzo ya Nje la Uswidi (EKN) umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 5-7 kila mwaka tangu mwaka 2000. 

Nchi zingine zenye uchumi imara kama Uswidi, yenye Pato la Taifa la dola bilioni 630, imepata ukuaji hasi mara mbili ndani ya miaka mitano iliyopita. 

Mnamo Julai 2020, Tanzania ilihitimu kutoka nchi za kipato cha chini na kuingia kwenye kundi la nchi za kipato cha kati, ambayo kwa mujibu wa Benki ya Dunia inaashiria maendeleo makubwa ya uchumi na utulivu kwa miongo miwili. 

Haya ni matunda ya mageuzi ya mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambayo yaliipeleka nchi katika uchumi mchanganyiko, na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, mchakato unaohitaji miongo kadhaa kukomaa.

Tanzania ilipokea korona za Uswidi milioni 560 mwaka 2024, takriban dola milioni 60 za Marekani, kama msaada kutoka Uswidi. Lakini Tanzania sasa inahama kutoka kwenye misaada kwenda kwenye biashara na uwekezaji; hivyo, inakaribisha wawekezaji wa Uswidi katika sekta muhimu kama viwanda, huduma, madini, utalii, kilimo na teknolojia.

Ni dhahiri kuwa, katika mwaka unaoishia Septemba 2025, Tanzania ilikusanya dola bilioni 4.43 kutokana na dhahabu, bidhaa inayoongoza kwa mauzo ya nje nchi, huku ikitarajia utalii utaleta dola bilioni 6.0 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025. 

Tanzania kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa utalii wa mbugani kwa mwaka wa tatu mfululizo, ikijivunia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro na fuko maridadi za Zanzibar.

Tanzania ina hifadhi kubwa ya madini muhimu ikishika nafasi ya tatu barani Afrika na ya sita duniani. Ufini inatusaidia katika utafutaji na utafiti wa utajiri huu wa kipekee, ambao kwa hakika 

utainua uchumi wetu. Uswidi inahimizwa kutumia fursa za kujenga mitambo ya kuchenjua madini nchini.

Mwaka 2024 pekee, Tanzania ilivutia uwekezaji wa moja kwa moja wenye thamani ya dola bilioni 9.31 kutokana na miradi 901 iliyosajiliwa, na nchi hii inajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 140.

Pamoja na mafanikio haya, serikali ya sasa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mikakati zaidi ili kuwaletea Watanzania maendeleo thabiti na endelevu.

Hivyo basi, kwa dhati kabisa, kwa uchumi wenye sekta nyingi na unaofuata soko huria huku

ukionesha ukuaji stahimilivu wa kuvutia, kuibagaza Tanzania kwamba "imelowea kwenye Ujamaa 

usio na maendeleo" si sahihi na ni upotoshaji.

Mwandishi ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za Nordic, Baltic na Ukraine, mwenye makazi yake Stockholm.

Share:

Tuesday, 16 December 2025

KARAKANA YA KISASA YA BIDHAA ZA NGOZI YAJA KUIBADILISHA SEKTA YA NGOZI NCHINI


..

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amemtaka Mkandarasi wa COMFIX & ENGINEERING kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano Afika Mashariki (EASTRIP ) katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza, ili ikamilike kwa wakati kulingana na maktaba.

Naibu Waziri huyo, ametoa maagizo hayo jijini Mwanza wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo. Pia amewataka wazabuni wote kuhakikisha vifaa na mitambo vinawasili na kufungwa kwa wakati ili kuwezesha utoaji wa mafunzo kwa wakati.

Mhe. Wanu Ameir amesema ucheleweshaji wa ujenzi unaweza kuathiri malengo ya Serikali ya kuhakikisha vijana wanapata ujuzi na umahiri unaohitajika katika soko la ajira la ndani na kimataifa, kama alivyoelekeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Ameir amewahakikishia wananchi na uongozi wa DIT kuwa Serikali itaendelea kuimarisha uwezo wa kampasi hiyo, ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 358 wa sasa hadi 2,000

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema kuwa katika Kampasi ya DIT Mwanza kinajengwa Kituo cha Kikanda cha Umahiri cha uchakataji na utengenezaji wa bidhaa za Ngozi ambacho kinatekelezwa kupitia Mradi wa EASTRIP. Amesema kuwa ujenzi huo unahusisha majengo matano ambayo ni jengo la kufundishia, jengo la taaluma, hosteli mbili na karakana ya kisasa kwa ajili ya mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi.

Prof. Mushi ameongeza kuwa ujenzi wa majengo hayo unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ambayo imetoa mkopo wa riba nafuu kufanikisha mradi huo. Ambapo gharama za utekelezaji wa mradi DIT Mwanza ni shilingi bilioni 37.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam (DIT) Kampasi ya MWANZA Dkt. John Msumba amesema kuwa Kampasi hiyo imefufua Sekta ambayo ilikuwa imekufa nchini kutokana na kukosekana Kwa wataalamu na kwamba Viwanda Kwa sasa vinapata wataalamu tofauti na awali ambapo walikuwa wakilazimika kuwatoa nje ya nchi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger